Malipo ya Ada
Ndugu mzazi/mlezi, napenda kukumbusha kufanya malipo ya ada ya mwanao kabla ya kufungua shule tarehe 12/04/2021. Hivyo unahimizwa kufanya hivyo ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza baada ya tarehe ya mwisho. Sambamba na hilo pia unapaswa kumalizia ada (Kama bado unadaiwa) ni kwa ajili ya kukamilisha malipo ya ada ya Muhula wa kwanza ,kwani pasipo malipo hayo mwanafunzi hatapokelewa shuleni.
Malipo yote yatatakiwa kufanyika katika benki ya NMB kwa kutumia A/C No 30410026649 jina la akaunti ni HOPE COMMUNITY DEVELOPMENT.
Ada kwa wanafunzi wa bweni ni Sh. 1,300,000/= na kwa wanafunzi wa kutwa ni Sh. 950,000/= kwa mwaka.
Mahitaji mengine ni:-
- -Ziara ya kimasomo [study tour] kwa kidato cha pili Sh. 100,000. Ni lazima pesa hii kulipwa kabla ya mwanafunzi kuja shuleni
- -Wanafunzi wote watapaswa kuja na barakoa za vitambaa zisizopungua mbili na kila mwanfunzi ahakikishe ana vyombo vya chakula ambavyo ni sahani na kikombe cha rangi ya kijani
- -Rimu moja aina ya Double A na si vinginevyo kwa wanafunzi wote wa kidato cha tatu na vidato vingine ambao hawakuleta Januari.
MUHIMU
- -Hakutakuwa na likizo ya mwezi wa sita kwa wanafunzi wa kidato cha pili na cha Nne hivyo mzazi unapaswa kuchangia pesa kwa ajili ya chakula kwa huo muda wa likizo kiasi cha Sh.120,000/=.
Kwa mawasiliano zaidi na maswali mengine tafadhali piga namba 0766 787 193
Imetolewa na Meneja wa Shule.
News
-
March intake - we are receiving new applications
Released: 14/01/2024 | ManagerArusha public College informing their customer hat new intake has opened
-
Tuition fee
Released: 26/03/2021 | College DirectorTuition fee should be paid via college Bank account
Announcement
-
Joining Instruction